FULL VIDEO : UFUNGUZI WA DSE SCHOLAR CHALLENGE 2017, ULIOFANYA NA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA



Nimekuekea hapa mkusanyiko wa matukio yote yaliyotokea kwenye uzinduzi wa DSE SCHOLAR CHALLENGE 2017 ambapo Chuo Cha Uhasibu kilikua ndio wafunguzi..


DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE ni shindano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya Wanafunzi wote wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Shule za Sekondari Nchi Nzima. Shindano hili linaratibiwa na kuendeshwa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kila mwaka kuanzia tarehe 1 Aprili hadi tarehe 30 Juni.


 
Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 limedhaminiwa na CRDB Bank; SWISSPORT Tanzania; na FSDT. Vile vile mfumo wa ushiriki katika hili shindano kwa njia za simu na internet umewezeshwa na Mitikaz Limited na Maxcom Africa.
 
Kwa mara ya Kwanza Shindano la mwaka huu litashirikisha Wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Shindano Maalum la Uwekezaji kwa kupitia mfumo wa kiTeknohama unaofikiwa kwa njia ya tovuti ya www.younginvestors.co.tz.
 
Wanafunzi wanaweza kushiriki kwenye hili shindano BURE:
  1. Kupitia tovuti ya www.younginvestors.co.tz
  2. Kupitia Application ya Smartphone ya Leverage Scholar
  3. Kupiga namba ya simu ya *150*36#  

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.