MAN UNITED AND JOSE MOURINHO MATCH MADE IN HEAVEN ??
Usiku
wa kuamkia Tarehe 25/5/2017 moja kati ya waimbaji maarufu nchini
Tanzania,omary Nyembo almaarufu ommy dimpoz alionekana ameshikilia simu
yake akiimba jose mourinho,josee mourinho,akiwa miongoni mwa ma elfu wa
mashabiki waliojitokeza katika dimba la friends arena kushuhudia Man U
ikimenyana na Ajax Amsterdam kuwania kombe la europa league.
Yes
it was Jose mourinho again,hivi ndivyo unavyoweza kusema,nani asiye jua
kua mreno huyu ni mshindi? Wapi ambako hajawahi kushinda? Porto?
Chelsea? Inter? Madrid? Chelsea tena? Popote ambako josee aligusa nyayo
zake aliondoka akiwa mshindi huyo ndo josee mourinho.
Katika
msimu wake wa kwanza pamoja na manu kuto onekana kama ni timu bora
lakini josee mourinho amefanikiwa kuweka kabatini makombe mawili,kama
utaamua kujumlisha na ngao ya jamii unazungumzia makombe matatu! Baada
ya fergie hakuna kocha ameonyesha mafanikio hayo zaidi ya jose mourinho!
Achilia
mbali kejeli zake,maneno yake ya shombo kwenye press
conferences,mourinho ni mmoja kati ya makocha wa kizazi hiki ambaye
unaweza kusema kua naye kwenye team yako basi tayari una makombe kwenye
kabati,mourinho anajua kupiga hesabu na kunusa njia za kuchukua kombe.
Katika
wakati ambao man United walionekana kutokua na mwelekeo wowote kwenye
league,mourinho alinusa kua mafanikio yapo Europa ivo akarisk ligi kuu
na kukubali kupoteza baadhi ya mechi kwa kukaza europa ligi leo kila
mmoja ameshuhudia hesabu kali za jose mourinho.
Mwana
Fa katka nyimbo aloshilikishwa na bilnass Ana mstari unasema mwandiko
mzuri sio lazima bwana we andika mengine tutaona,ndivyo unavyoweza
kusema kwa mourinho hawajaonesha mchezo mkubwa wa kuvutia lakini tumeona
alichokipata pamoja na kutokua katika kiwango kikubwa.
Is
this match made in heaven? Tusubiri tuone,lakini kuna dalili njema kua
Man U wamepata mrithi sahihi wa sir Alex ferguson,bado kuna kazi kubwa
ya kufanya kuhakikisha Manu inarudisha hadhi yake kama ilivyo kua miaka
ya nyuma,lakini josee mourinho anatupa imani kua upele umempata mkunaji.
No comments:
Post a Comment