" NIMEFUNDISHWA KUSHUKURU " - MISS TANZANIA 2016 AWAJIBU WANAOLISEMA GARI LAKE
Miss Tanzania 2o16 Diana, baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aliloahidiwa kufuatia ushindi kwenye shindano lililofanyika October 2016, gari hilo limekuwa gumzo mitandaoni kutokana na mabango yaliyowekwa kwenye gari hilo.
Diana ameyazungumza haya...
“Mabango yatatolewa siku hizi mbili na nimefundishwa kushukuru. Kwa hiyo, nilichopewa nimeshukuru. Nitaliendesha gari, sina kipingamizi. Maneno, watu watayaongea, hiyo ipo. Hakuna binadamu anayekubali kitu. Ndio uwezo wao ulipofikia wa kunipa hiyo zawadi.
“Siwezi kuwapinga – ninawaunga mkono. Mimi ni binadamu pia, kwa hiyo, nimepewa zawadi na nimepokea kwa shukrani, na nawashukuru Kamati na wadhamini na watu wote walioshiriki mpaka nikapata gari.
“Sijui wanachokiongea, ila hali halisi ndio hiyo. Niliitwa nikaambiwa gari lako ndio hili. Nikalipokea kwa shukrani. Mimi sijali watu wanasema nini, maana maneno yapo. Wao wamenipa walichokiweza kwa sababu wamehangaika kweli kulitafuta hilo gari. Watu hawawezi kujua kwa sababu wapo kwenye social media, lakini wangekuwepo tangu watu wanahangaika kulipata hilo gari tangu mwezi wa 6 mpaka leo hii wmaepata.”
No comments:
Post a Comment