NUSU FAINALI UEFA : REAL MADRID VS ATLETICO MADRID , MECHI NYINGINE ITAKAYOSIMAMISHA DUNIA LEO,, TAZAMA TAKWIMU HIZI



Mnamo miaka mitatu kabla ya Tanzania kupata uhuru, mechi kama ya lo ilifanywa ikiwa ni nusu fainali kati ya Real madrid na Atletico 
Real Madrid waliifunga Atletico katika mchezo huo kwa bao 2 kwa 1 mabao ya Real Madrid kipindi hicho yakifungwa na Ferenc Puskas na Jose Hector huku bao la Atletico ambao walitangulia kufunga likiwekwa kimiani na Antonio Alvarez.
Baaadae Real Madrid walipanda basi kuwafuata Atletico katika mchezo wa marudiano ambapo Atletico walishinda kwa bao 1 kwa 0 kwa bao la Enrique Collar ambapo baada ya matokeo haya ilizifanya timu hizi kucheza mechinya playoff ambapo Real waliitoa Atletico kwa bao 2 kwa 1.
Toka kipindi hicho mwaka 1958 hadi leo hii Real Madrid wamekuwa wakiionea Atletico Madrid kwani walikutana katika fainali ya UEFA mwaka  2015 Real wakaibuka kidedea na wakafanya hivyo tena katika fainali ya mwaka 2016.
Lakini Zinedine Zidane kocha wa Real Madrid haamini kama vipigo walivyowapa Atletico ni sababu ya wao kuingia leo wakiwa kifua mbele, Zidane ambaye atamkosa Gareth Bale leo ametoa onyo kwa wachezaji wake.
Image result for uefa half final 2017 real madrid and atletico
“Hatuwezi kukumbuka yaliyotokea hayo yalipita, naamini(Atletico) watakuja wakiwa wamejiandaa sana kuweza kutukabili, sio mchezo rahisi hata kidogo, mara zote wamekuwa wagumu sana kwetu na kila mwaka wanakuwa bora zaidi” alisema Zidane.
Kwa upande wa Atletico kocha Diego Simeone amesema anaamini wachezaji wake leo watamfanya ajivunie kuwa nao, “nawaamini sana na naamini wataonesha kiwango kitakachonifanya nijivunie kuwa nao” alisema Simeone.
Wakati Real Madrid wanamkosa Gareth Bale, kwa upande wa Atletico watawakosa Juanfran na Jose Gimenez huku fundi wao wa mpira Yannick Carrasco naye akiwa kwenye hatihati kulikosa pambano hilo.
Swali kubwa kwa mashabiki wa Real Madrid wanalojiuliza ni nani atakaa nafasi ya Bale? Lakini kiwango cha kinda Asensio linaweza kuwa jibu la Real Madrid huku pia kiwango cha Isco kinaweza kuwa jibu lingine kwa Los Blancos.
Atletico wanaonekana nao wameimarika kila idara lakini uwezo wa golikipa wao Jan Oblak unaweza kuifanya safu ya ushambuliaji ya Real Madrid kufanya kazi ya ziada kuweza kuutumbukiza mpira katika nyavu za Atletico.
Image result for uefa half final 2017 real madrid and atletico
Vikosi vinaweza kuwa hivi Real Madrid Navas,Carvajal,Nacho,Sergio Ramos,Marcelo,Toni Kroos,Casemiro,Modric,Ronaldo,Benzema,Isco huku Atletico wanaweza kuanza na Oblak,Stefan Savic,Hernandez,Godin,Filipe Luis,Koke,Saul Niguez,Gabi,Yannick Carrasco,Torres na Antoine Griezman.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.