" BEN POL AKINIKATAA, NITAJIUA KWA AJILI YAKE " - EBITOKE

Tokeo la picha la Ben Pol na ebitoke

Aliyesema mahaba niue hakukosea kabisa kwani hii imekuja kujidhihirisha kwa mchekeshaji mrembo Ebitoke ambaye karibia mwezi mmoja sasa anahangaika kuwinda penzi la Ben Pol.

Ebitoke amesema kwa sasa mahaba yake yote yapo kwa Ben Pol na endapo atashindwa kupata penzi lake basi yupo tayari kupoteza uhai wake.
“Hapana Ben Pol hawezi kuacha kuwa na mimi, nitafanya kila njia ili aweze kuwa na mimi ,”amesema Ebitoke huku akisisitiza kuwa yupo tayari hata kujiua kwa ajili ya Ben Pol.
Hata roho nitaweza kujitoa….ndiyo nitajiua kwa ajili yake.. ndiyo nitajiua kwa ajili yake… sitofanya dhambi kwa kujiua kwa ajili yake,”amesema Ebitoke kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo mrembo huyo mchekeshaji haswaa amesisitiza kuwa watu wasishangae maamuzi yake ya kujiua endapo atakataliwa na Ben Pol kwani mapenzi ni upofu na yana hisia kali moyoni.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.