NEYMAR KUTAMBULISHWA LEO RASMI PSG ,,, TAZAMA ALICHOSEMA
Klabu ya Paris St-Germain wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Brazil, Neymar kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya Euro milioni 222 sawa na pauni milioni 200 kutoka Barcelona.
Ununuzi huo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 umevunja rekodi ya awali iliyowekwa na Paul Pogba aliporejea Manchester United kutoka Juventus kwa pauni milioni 89 mwezi Agosti 2016.
Neymar atakuwa analipwa Euro milioni 45 sawa na pauni milioni 40.7 kwa mwaka nakulipwa Euro 865,000 sawa na pauni 782,000 kila wiki hii ikiwa ni kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya pauni milioni 400.
Neymar amesema amejiunga na “mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi Ulaya”.
“Ndoto kuu ya Paris St-Germain ilinivutia kujiunga na klabu hiyo, pamoja na kujitolea kwao na nguvu zinazotokana na hili”. Najihisi niko tayari kuanza kazi. Kuanzia leo, nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya.” Amesema Neymar.
Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa imepanga kuwa na kikao na wanahabari leo siku ya Ijumaa
Neymar atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG Jumamosi wakati wa mechi yao ya kwanza kabisa ya msimu mpya, ambapo watakuwa katika uwanja wa nyumbani wa Parc des Princes wakicheza dhidi ya Amiens.
No comments:
Post a Comment