TAHADHARI: VIRUSI VYA ZIKA NI HATARI ZAIDI

Mbu asambazaye virusi vya Zika

Wanasayansi nchini Brazil wamesema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali.

Madaktari bingwa wameiambia BBC kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.

Madaktari wengi na watafiti sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye ubongo.

Lakini wakati asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na virusi vya Zika wakati wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye vichwa vidogo.

 Madaktari nchini Brazil wamesema kuwa asilimia ishirini ya mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya kuharibiwa kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.

Kasi ya maambukizi katika baadhi ya sehemu nchini Brazil imepungua kutokana na elimu iliyotolewa kuzuia maradhi hayo, hata hivyo hati hati za kusaka chanjo ya kupambana na Virusi bado ziko katika hatua za awali, huku hatari ikiendelea kuwepo katika ukanda wa Amerika ya kusini.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.