MAFUNDI WA SIMU WABANWA.... CHAMA CHA MAFUNDI WA SIMU KUPEWA ELIMU

CHAMA cha Mafundi Simu nchini kimesema hakitamfumbia macho fundi yeyote atakayehusika katika kuharibu mfumo wa rajisi za utambulisho katika simu baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) kuzima simu feki usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa semina ya wadau wa mawasiliano kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, Mwenyekiti wa chama hicho, Gwakisa Mwakatika alisema ni lazima kila fundi afuate taratibu na weledi wa kazi na kuacha kujihusisha na kuharibu mfumo wa rajisi za utambulisho na wizi.





No comments:
Post a Comment