HILLARY CLINTON KUWEKA HISTORIA MPYA MAREKANI




Hillary Clinton ambaye ni mwanamama wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais wa chama kikubwa baada ya kupitishwa kuwa mgombea wa Chama cha Democratic, ameandika historia baada ya kupitishwa na wajumbe 2,382 waliohitajika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuhesabu kura za majimbo yaliyokuwa yamesalia.

Clinton ambaye sasa amekubali rasmi kuwania kiti cha urais nchini humo amesema wakati wa kupambana na mpinzani wake sasa umeanza rasmi huku akiwataka wanachi wa Marekani kumuunga mkono kwani yeye pekee ndiye anayeweza kusuluhisha matatizo ya nchi hiyo.

Kutokana na umahiri alionao mwanamama huyo kumepelekea kuungwa mkono na watu mashuhuri akiwemo Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton pamoja na Rais anayemaliza muda wake Barack Obama kwa kusema “Hakujawahi kuwa na mwanaume au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa rais kama Hillary Clinton”.

Endapo mwanamama huyu atafanikiwa kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo ataandika historia kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Marekani na kuingia katika rekodi za dunia kwa kuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kuwa marais.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.