SHAFFIH DAUDA AMEELEZA DONDOO 10 MUHIMU KABLA YA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO - PSG VS ARSENAL

2

Leo kivumbi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kinaendelea kwa michezo ya nane kwenye makundi manne kupigwa katika viwanja tofauti-tofauti.

Mchezo unaovuta hisia ya watu wengi ni mchezo wa Kundi A kati ya Paris Saint Germain na Arsenal utakaopigwa kunako Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris.

Dondoo muhimu za kuzingatia kuelekea mchezo huo: : 
  • Mara ya mwisho Paris Saint-Germain kukutana na Arsenal ilikuwa msimu wa 1993/94 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Cup Winners Cup, ambapo Arsenal walishinda kwa wastani wa mabao 2-1.
  • Arsenal hawajafungwa katika michezo yao 12 ya ugenini dhidi ya timu za Ufaransa kwenye Michuano ya Ulaya. Wameshinda michezo saba ya mwisho.
  • Hii ni mara tano mfululizo kwa kwa PSG kushiriki Champions League na mara ya tisa kwa ujumla. Lyon pekee ndio wamewazidi ushiriki kati ya timu zote za Ufaransa (mara 14).
  • Arsenal wamefuzu kwenye Champions League kwa mara ya 19 mfululizo, wakizidiwa na Real Madrid tu ambapo wameshiriki mara 20 mfululizo.
  • Arsenal wameweza kufuzu kwenda hatua ya makundi misimu 13 mfululizo iliyopita lakini wamekuwa wakitolewa kwenye hatua ya 16 bora kwenye misimu sita mfululizo.
  • Wamewahi kufika fainali mara moja tu (mwaka 2006) na kufungwa mabao 2-1 na Barcelona.
  • Petr Cech ameweza kupata clean sheets 47 kwenye michezo 111 ya Champions League. Amezidiwa na Iker Casillas (mara 51) na Edwin van der Sar (50) pekee.
  • Miongoni mwa magoli 13 yaliyopita kwenye Champions League yaliyofungwa na Arsenal, Alexis Sanchez amefunga mara tatu na kutoa pasi za magoli 5.
  • Akiwa kama meneja, Wenger amecheza mechi 176 za Champions League, nyingi zaidi ya kocha wowote kwa sasa. Ni Ferguson pekee ndio amemzidi (amecheza mechi 190)
  • Kwenye Michuano ya Euro mwaka huu, Arsenal walikuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha Ufaransa zaidi ya wapinzani wao. Arsenal walikuwa na Olivier Giroud na Laurent Koscielny wakati PSG walikuwa na Blaise Matuidi ambaye alicheza takriban michezo  yote

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.