JE, ARSENAL ITAWEZA KUPITA NA KULIPIZA KIPIGO CHA 5 - 1 DHIDI YA BAYERN LEO? TAZAMA TAKWIMU HIZI


Image result for uefa arsenal vs bayern
Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, zinaanza kuchezwa leo Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.
Huko Emirates Jijini London, Wenyeji Arsenal wanapaswa kupindua kipigo cha 5-1 walichoshushiwa na Bayern Munich katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Ujerumani.
Ili kufuzu kuingia Robo Fainali, Arsenal wanapaswa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika kwa kushinda 4-0 au kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 4-0.
Image result for arsenal vs bayern uefa
Mechi ya Pili ya leo ni huko Naples, Italy wakati Napoli ikirudiana na Mabingwa Watetezi ,Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa bao 2-0 kwa kuwa mchezo wa awali walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain kwenye Mechi ya Kwanza.
Napoli pia wanaweza kufuzu ikiwa watashinda kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 2-0.
Image result for uefa round 16
Kesho ,Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 ; Barcelona na Paris Saint Germain,huku PSG wakiwa mbele 4-0 na mechi ya pili ni kati ya Borussia Dortmund na Benfica huku Benfica wakiongoza 1-0.
Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitakamilika Wiki ijayo, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza Robo Fainali.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.