STEVE NYERERE - " PANYA NI KIUMBE MJANJA SIO PAKA ANYESUBIRI KUPEWA, TID NI PAKA"




Msanii wa filamu za vichekesho Steve Nyerere aliyeambiwa yeye ni panya na TID, muigizaji huyo ameibuka na kujibu mapigo.

Wawili hao walianza kutupia maneno kutokana na sakata la madawa za kulevya baada ya muigizaji huyo kudai TID alilipwa milioni 2 na RC Makonda kuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu issue ya yeye kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Muigizaji huyo alidai yeye hawezi kuanza kujibishana na TID kwa kuwa TID si kitu chochote.
“Siwezi kubishana na TID ambaye akiona gari yangu analikimbia apate chochote kitu. Kwahiyo nikianza kubishana naye nitakuwa napoteza muda, halafu mimi na TID ni kama vidole kuna kikubwa na kidogo yeye wakati wake ulishapita huu ni wakati wa Steve lazima ajenge heshima,” Steve Nyerere alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza “Alivyonifananisha na panya nimependa kweli, kwanza namsifu kwa sababu amenifananisha na kiumbe mjanja. Kwahiyo mimi nasema bora mimi panya kuliko yeye paka ambaye anasubiri atengewe ale, nimefurahi sana kwa sababu amenisifia kunifanisha na mnyama mjaja,”.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.