KUTANA NA ROBOTI ANAYEFANYA KAZI ZA KISHERIA - " WAKILI ROBOT "

Wakili roboti

Awali teknolojia ilitumiwa kukabiliana na faini za makosa ya bara barani sasa inawasaidia wakimbizi wenye madai ya kisheria.
Wakati Joshua Browder alipotengeneza DoNotPay aliita " Wakili roboti wa kwanza duniani".
Ni chatbot -programu ya kompyuta inayofanya mazungumzo kwa njia ya ujumbe na maagizo ya sauti - na inatumia ujumbe wa Facebook wa Messenger kukusanya taarifa juu ya jambo na kutoa ushauri pamoja na nyaraka za kisheria.
Awali iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi.
Joshua Browder aliyebuni programu ya DoNotPay
Lakini sasa Browder - Muingereza mwenye umri wa miaka 20-ambaye sasa anasoma katika chuo kikuu cha Stanford nchini Uingereza - ameweza kuwezesha roboti yake kuwasaidia wanaoomba uhamiaji.
Nchini Marekani na Canada, inawasaidia wakimbizi kukamilisha maombi yao ya uhamiaji, na nchini Uingereza, inaweza kuwasaidia wanaoomba uhamiaji katika kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa serikali.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.