SAMATTA KAFANYA YAKE USIKU WA ULAYA JANA,,, KATUPIA MBILI



Mbwana Samatta kafanya yake kwenye usiku wa Ulaya wakati klabu yakeya KRC Genk ikicheza mchezo wa kwanza wa 16 bora wa michuano ya Europa League dhidi ya Gent.

Samatta akiwa katika kiwango cha juu ameweka kambani bao mbili katika mchezo huo uliomalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Gent ambao ni wapinzani wao kutoka kwenye ligi kuu ya Ubelgiji.

Samatta kafunga goli lake la kwanza kwenye mchezo huo huku likiwa ni goli la tatu kwa timu yake dakika ya 41 akipokea pasi ya Boetius kwa kuuweka mpira kifuani kisha kuachia bakora kali kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya penati box.

Dakika ya 72 nahodha wa Tanzania akaweka kambani bao lake la pili kwenye mchezo huo huku likiwa ni bao la tano kwa Genk akiitendea haki pasi ya mwisho ya Thomas Buffel akiwa ndani ya sita na kuiweka timu yake kwenye mazingira mazuri ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.