RAIS JPM AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA RC MAKONDA, AMEYASEMA HAYA LEO

Image result for magufuli

''Kampeni zilishakwisha. Ulie ugaregare, Rais ni Magufuli. Ndio maana hii interchange inajengwa kwenye jimbo la CHADEMA, nawaomba watanzania wa vyama vyote tujifocus kwenye suala la maendeleo.

Mnahangaika mnapost kwenye vipost vyenu, mpaka watu wengine wanaingilia uhuru wangu. Mimi huwa sipangiwi mambo. Mimi ni Rais ninayejiamini, siwezi kupangiwa, hata siku ya kuchukua fomu nilienda mwenyewe.

Nitaamua mwenyewe nani akae wapi, kwahiyo Makonda wewe chapa kazi, nasema chapa kazi. Najua wamenielewa. Kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi naandikwa kwenye mitandao, Kwahiyo nijiuzulu Urais?

Mimi ningefurahi hata kwenye mitandao tungekuwa tunapata ushauri jinsi ya kufanya, tunajadili personality na sio ideas, tuchape kazi kwa manufaa ya watanzania''. 


Hayo ni maneno ya Rais John P. Magufuli mchana wa leo wakati akizindua Mradi wa Fly Over katika makutano ya barabara ya Ubungo jijini Dar es Salaam.



No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.