" TUNASUBIRI KUSIKIA KUTOKA KWA PAUL MAKONDA, TIMU YA WATU 5 IMEUNDWA " - NAPE NNAUYE

Image result for nape nnauye

Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi haijapinduliwa.

Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.


Watu wengine mbalimbali wameandika na kusema haya pia...

 Waziri Nape: 

Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi

Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya

Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24\

Kusaga: 

Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!

Reginald Mengi: 

Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.