ASKOFU GWAJIMA ADAI KUTISHIWA KUUWAWA KUPITIA UJUMBE MFUPI WA SIMU

Image result for gwajima

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu huku akidai kuwa watu waliomtumia ujumbe wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi na kuusambaza kwa watu.
Askofu Gwajima ameyasema hayo katika ibada yake ya Jumapilii, amesema kuwa baada ya kuupata ujumbe huo alifanya maombi kwa ajili ya kuwafuta waliomtumia na kujua kinachoendelea.
“Kuna Askofu anajiita Nabii mdogo juzi alikuwa anasambaza meseji anasema naona Gwajima anamaliza mwendo wake,utamaliza mwendo wako mwenyewe, 
nimeapa kwa jina la bwana yeye anayesema nitamaliza mwendo kwa nguvu za giza atamaliza yeye kwanza na siyo mimi kwa jina Yesu na wiki ijayo ataumaliza mwendo yeye mwenyewe kwa jina bwana. 
Nimeapa kwa jina la baba kama yeye alivyotamani watu wamalize mwendo kwa maslahi ya mwendo wa giza na wewe umalize mwendo kwa maslahi ya ufalme wa Yesu kristo usiharibika kwa jina la Yesu kristo,” alisema Gwajima.
“Jana nilikuwa namsaka aliyetuma meseji hiyo kwenye makorido ya kiroho, nikamuona, mimi nina agano na Bwana kwamba adui zangu wakija kwa njia moja wataondoka kwa njia saba, silaha zote zitakazokuja kwangu hazitofanikiwa, yeye ndiye atakayekufa siku ile ile aliyoipanga, siyo mimi.”

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.