RAIS JPM ATOA ZAWADI ZA EID EL FITR KWA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA


Rais Magufuli atoa zawadi ya Eid El Fitr kwa watoto Mahabusu Arusha, ambapo katibu tawala Mkoa, Richard Kwitega amekabidhi zawadi  za Eid kwa mahabusu ya watoto kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania. 

" Mheshimiwa Rais ametoa zawadi mbuzi dume, mchele kilo 25 na mafuta yakupikia lita 10. vitu hivyo vitawasaidia watoto hao katika sikukuu hiyo " Alieleza Ndugu Kitwega.

Aidha, amewapa salamu za Rais kwa kuwataka wajue mahali pale ni pa muda mfupi tu hivyo wakitoka wanatakiwa wakawe raia wema na wakujituma zaidi katika kazi na wale ambao ni wanafunzi wkakazane na masomo yao. 

Wakitoa shukrani zao kwa Rais, watoto hao wameeleza, n kuiomba serikali kuwasaidia usikilizwaji wa kesi zao zisichukue muda mrefu sana na hivyo kupelekea wengi wao kukosa masomo yao ya shule. 

Mkurugenzi wa kituo hicho Musa Mpua, amesema tokea mwaka huu uanze ni watoto 48 wameshapitia katika kituo hicho na kwa sasa wapo watoto 11 tu na wote ni wa kiume. Changamoto kubwa wanayo pitia ni ukosefu wa gari la kubeba watoto hao pale wanapoitajika kupelekwa mahakamani n ukosefu wa uzio kwa usalama wa watoto.

Kila mwaka Mheshimiwa Rais amekuwa akitoa zawadi mbalimbali za Eid katika maeneo mengi ya nchi kwa lengo la kushiriki na walengwa katika kusherehekea sikukuu.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.