PAMBANO LA MAYWEATHER VS MCGREGORY KUVUNJA REKODI UPANDE WA FEDHA.



Floyd Mayweather vs. Conor McGregor ni pambano ambalo litafafanua vizuri maana ya tukio tajiri la kimichezo mnamo August 26 wakati pambano hili litakapovunja rekodi zote za kifedha zilizowahi kuwekwa huko nyuma katika mchezo huu wa ndondi.

Mnamo mwaka 2015, pambano la Mayweather vs. Pacquiao lilizalisha kiasi cha zaidi ya $600m – sasa tegemea pambano la Mayweather vs. McGregor kutengeneza namba kubwa zaidi ya hizo wakati litakapoonyeshwa kupitia malipo ya kuangalia kwenye TV.

Jarida la Forbes linaripoti kwamba pambano hili litaingiza karibia $1billion – wanasema japokuwa hawajapata namba kamili ila hili ndio litavunja rekodi zote za huko nyuma.

Zaidi ya mashabiki 48,000 walikusanyika katika kumbi za Staples Center, Budweiser Stage, Barclays Center na Wembley Arena kuangalia mikutano ya waandishi wa habari iliyowahusishwa miamba hiyo ya ngumi.



Zaidi ya watu millioni 33 waliangalia mikutano hii kupitia mtandao wa Youtube ulimwenguni kote. Hii yote inakupa picha mvuto mkubwa uliolizunguka hili pambano.

Kampuni yoyote inayotaka kuwa mdhamini wa pambano hili inabidi ajiandae kulipa kiasi kikubwa cha fedha, kwa mujibu wa taarifa kimo cha chini kujitangaza katika pambano hilo ni $10 million sawa na 20 Billion za kitanzania. 



Kampuni ya vinywaji ya Tecate walilipa kiasi cha $5.6 million kuwa mmoja wa wadhamini wakubwa wa pambano la Mayweather vs Pacquiao. Kampuni ambayo inakuwa mmoja wa wadhamini wa juu inapata nafasi ya logo yake kukaa katikati ya ulingo katika uwanja wa T-Mobile Arena. Pia kampuni inapata nafasi ya kuwavalisha mavazi yenye logo zao wasichana wa ulingoni, kamba 2 za ulingo na kona ambazo mabondia hawakai. (Neutral corners)

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.