WALICHOKIONGEA CHADEMA BAADA YA FREEMAN MBOWE KUTAJWA KWENYE LIST

Image result for chadema freeman mbowe

Makao makuu ya CHADEMA, Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari mara tu baada ya jina la mwenyekiti wa chama hicho kutajwa kwenye list ya Makonda na kusema yafuatayo :: 

Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani


Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita
Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.