" HAKUNA ATAKAYEKUJA KAMA MIMI " - NUKUU ZA RAIS JPM SINGIDA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaania, Dkt John Pombe Magufuli amezungumza mambo mbalimbali akiwa ziara mkoani Singida na leo amezindua barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa KM 89.3.

Tazama nukuu zake hapa:
-Kabla sijaongea chochote naomba tuwaombee Mashujaa wetu walioitetea nchi yetu. Naomba tuiname tuwaombee
-Watanzania naomba tuwe tunakumbuka mahali tulipo toka, mahali tulipo na mahali tunapoelekea
-Tanzania ninayoipenda ni Tanzania yenye umoja, Tanzania yenye upendo, Tanzania inayomtanguliza mbele Mungu
-Tunataka tuwe na umeme wa uhakika ili tuweza kuwa na Tanzania ya viwanda tunayoitaka
-Wakati wa kukaa kwenye magenge na kushinda kwenye pool kukaa kupiga stori kwamba tutaletewa chakula cha bure, hakuna.
-Utajiri hautakuja kwa wavivu, lazima niwaeleze ukweli. Niwaombe wana Itigi wakati wa kukaa kwenye magenge umepita
-Mimi ndiye Rais, hakuna anaejua siri za Serikali kama Rais. Leo mmepata Rais anaewaambia ukweli
Kosea hata kuoa, utatoa hata talaka ila usije ukakosea kuchagua
-Ukiona mtu anapiga kelele wananchi wake waendelee kuwa masikini ujue amemeza kitu ndani
-Kazi ya kutumbua ni ngumu unaweza ukajikata, unaweza ukarukiwa na usaa . Inadepend hilo jibu limekaa sehemu gani
-Na leo watoto wote wanakalia madawati awe wa Chadema awe wa Tundu Lissu anakaa
-Ni mataifa machache duniani yanayosomesha watu wake bure, hata Ulaya hawafanyi hivyo ndugu zangu
-Ndege ya abiria 262 yenye uwezo wa kusafiri moja kwa moja kutoka Marekani inakuja mwakani
-Waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza kuanza kubomoa taratibu nyumba zao
-Ma-DC na Ma-RC, sitoi chakula kama kwako kuna njaa, wilaya ikiwa na njaa wewe DC hufai kuwa DC, na wewe RC hufai
-Nataka Tanzania iwe kama Ulaya. Tutafika tu lakini tutabanana
– TanRoadS ni ya 3 kwa uchapaji kazi Afrika
-Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo, lakini kuacha kusema siwezi
-Nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.